Msanii wa kimataifa Diamond Platnumz ametumia ukurasa wake kuwahabarisha wapenzi wa muziki kuhusiana na Wasafidotcom ambao ni mtandao mpya wa kuweza kununua nyimbo za wasanii wa Tanzania na nje ya Tanzania.
THE POST
Habari Mashabiki zetu pendwa…tunayo furaha kukupa habari njema ya kwamba kuanzia sasa @wasafidotcom ndio sehemu rasmi na pekee ya kuweza kujipatia Nyimbo za wasani wako wote pendwa toka hapa nchini Tanzania nje ya Tanzania…lengo kuu la kuanzisha mtandao huu ni kuweza kuwarahisishia Mashabiki na wadau wa mziki wetu muweze kujipatia kazi za wasani wenu zikiwa zina Quality ama ubora sahihi, kirahisi na haraka…lakini pia kutusapot vijana ama watoto wenu nasi tuweze kuendelea kuwatengenezea kazi zenye ubora zaidi….
Lakini pia sababu nyingine ya kuamua kuanzisha mtandao huu ni jinsi mlivyokuwa mnatusapoti vijana wenu kwa kununua kazi zetu halaf mwisho wa siku baadhi ya wamiliki wa mitandao wakawa hawatupi haki zetu tunayostahili, yaani wakawa wanatudhurumu na kunufaika wao huku sie wasanii wenu tukiishia kuambulia umaarufu wa majina ila maisha yetu halisi “pangu pakavu”…hii ilituumiza na kutuliza sana, karibu miaka yote…..kwenye mtandao huu wa @Wasafidotcom tumeeka njia mbalimbali rahisi za kununua nyimbo, kupitia account ya simu yani Mfano: Vodapesa na mitandao yote ya simu Afrika, na pia kununua kwa njia ya Card ya Benki mfano: Master Card, Credit card, Visa card na njia zote za kibenki…. Matumaini yetu kuwa mtatusapoti kwa kununua kazi zetu @wasafidotcom….
na panapo majaaliwa kwa mara ya kwanza ijumaa ya kesho @Harmonize ataachia wimbo wake mpya Uitwao #NAMBIE na utakuwa unapatika @Wasafidotcom tu …. nitasikitika sana sana nikiona ama kusikia shabiki yetu wa damu ama mpemda muziki, anakuwa mtu wa kwanza kuomba kutumiwa nyimbo kwa bloototh ama Watsup badala ya kuingia @wasadidotcom kudownload….. kesho hiyohiyo pia kutakuwa Rasmi na App pamoja na nyimbo za wasanii wengine zaidi uwapendao…. @Wasafidotcom#WhereTheHitsBelong !!!!!! Mie nimewaekea ngoma zooote za tangu kale na zingine ambazo hamjawai kuskia, follow account Rasmi ya @Wasafidotcom ubonyeze link kwa bio ukapakue nyimbo uzitakazo
0 comments:
Post a Comment