Home » Events
Showing posts with label Events. Show all posts
Showing posts with label Events. Show all posts
Tuesday, September 5, 2017
Saturday, March 25, 2017
Diamond akusanya kijiji kwenye show ya Muscat
Usiku wa Ijumaa hii Diamond alifanya show kubwa ambayo ilihudhuriwa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza kutoka sehemu mbalimbali katika mji wa Muscat nchini Oman. Hizi ni baadhi ya picha za show hiyo.
Wednesday, March 22, 2017
Watu wakuta mawe ya makaburini kwenye nyumba zao alfajiri Bagamoyo
Bagamoyo watu wameamka
asubuhi wamekuta mawe ya makaburini (Mashahidi) yamewekwa
kwenye nyumba zao hali iliyozua taharuki huku baadhi yao wakidai yamewekwa na
mtu. Mwenyekiti
alikiri kutokea tukio hilo na kufanya utaratibu wa kuyarudisha mawe hayo
makaburini.
Monday, October 10, 2016
Chris Brown, Alikiba, Wizkid, Vanessa wanogesha tamasha la Mombasa Rocks
Wapenzi wa muziki mjini Mombasa, Kenya, Jumamosi hii walishuhudia moja ya matamasha makubwa zaidi kuwahi kufanyika. Tamasha la Mombasa Rocks, lilimdondosha msanii wa Marekani, Chris Brown kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki.
Alisindikizwa na Wizkid, Alikiba, Vanessa Mdee na wengine. Tazama baadhi ya show kwenye tamasha hilo.
Monday, September 19, 2016
Idris Sultan kuwania nafasi ya kuhost tuzo za MTV MAMA 2016
Mshindi wa shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwa mmoja kati ya wachekeshaji watakao host kwenye tuzo za MTV MAMA 2016.
Kupitia mtandao wa Instagram wa MTV wameandika, “Would you nominate@idrissultan to HOST @mtvmamas on 22.10.16 #mtvmama2016 NAY or YAY.”
Wasanii wengine wanaowania nafasi hiyo ni pamoja na Basket Mouth (Nigeria), Idris Elba (Uingereza) na Kelvin Hart (Marekani).
Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Jumamosi ya Oktoba 22 kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome, Afrika Kusini.
Tuesday, September 6, 2016
Kuizawadia Taifa Stars Dola 10,000 Za Marekani TFF Watuma Salamu Za Shukrani Kwa Gavana Wa Nigeria Kwa
Taifa Stars ilicheza mechi hiyo Jumamosi Septemba 3, 2016 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017). Katika mchezo huo ambao mashabiki waliingia bure, Taifa Stars ilifungwa bao 1-0 mara baada ya kuibana Super Eagles hivyo kumsukuma Gavana huyo kuandaa hafla ya chakula cha jioni ambako mbali ya kuizawadia Stars, pia aliizawadia Super Eagles dola 35,000 za Marekani.
Taifa Stars ilitua Dar es Salaam usiku wa kuamkiia leo Septemba 5, 2016 ambako baadhi ya wachezaji walipelekwa Hoteli ya Urban Rose, iliyoko katikati ya Jiji la Dar es Salaam wakati wengine hususani wale wa timu ya Azam FC walichukuliwa na viongozi wao kwa ajili ya safari ya kwenda Mbeya ambako Jumatano wanatarajiwa kucheza na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaofanyika Uwanja wa Sokoine mjini humo.
Kadhalika wachezaji wa Young Africans nao walichukuliwa kwa ajili ya safari ya kwenda Mtwara ambako watakuwa na mchezoi dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini humo wakati nyota wa Simba watabaki hapa Dar es Salaam kwani Jumatano itakuwa na kibarua dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Wakati nyota 18 wakitua Dar es Salaam, Nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta aliishia Nairobi, Kenya ambako aliunganisha ndege ya kwenda Brussels, Ubelgiji.
Licha ya mchezo huo kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini ulikuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kwa fainali hizo kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.
Wachezaji waliotua ni
Makipa-
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC
Mabeki
Vicent Andrew – Young Africans
Mwinyi Haji – Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe – Azam FC
David Mwantika – Azam FC
Viungo
Himid Mao – Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi – Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania
Washambuliaji
Jamal Mnyate – Simba
Simon Msuva – Young Africans
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco – Azam FC
Mbwana Samatta –KRC Genk ya Ubelgiji
Viongozi waliofika Dar ni:
Ahmed Mgoyi – Mkuu wa msafara
Charles Boniface Mkwasa- Kocha Mkuu
Hemedi Morocco – Kocha Msaidizi
Hussein Swedi – Mtunza Vifaa
Richard Yomba – Daktari wa timu
Monday, September 5, 2016
Vanessa Mdee atumbuiza na 2 Face kwenye show ya Buckwyld N Breathless, Lagos
Katika sehemu ambayo Vanessa Mdee ameshalikita jina lake vyema nje ya Tanzania, basi ni Nigeria.
Vee ambaye alitengeneza pair iliyovuma zaidi kwenye Coke Studio Afrika mwaka jana na 2 Face, hakuwa mchoyo wa fadhila kumshukuru muimbaji huyo kwa nafasi aliyompa.
“This picture describes everything I was feeling last night,” ameandika Vanessa kwenye picha akiwa na 2 Face jukwaani aliyoiweka Instagram.
“I thankyou @official2baba for constantly inspiring and elevating youngns like myself. I’m humbled and eternally gratefully.”
2 Face amewahi kukaririwa akimtaja Vanessa kuwa ni mmoja wa waimbaji anaowakubali Afrika.
Saturday, September 3, 2016
Wiz Kid At Fiesta 2016 Mwanza
Najua kuna list kubwa ya watu wangu ambao walikuwa na hamu kushuhudia mambo yalivyokuwa kwenye stage ya FIESTA 2016 ambayo imeanza ziara yake mikoani kwa sasa na ilianzia Mwanza August 20 1016 ambapo palikuwa na list ndefu ya wasanii kutoka bongoflevani na pefomance ya msanii kutoka Nigeria
Site Users
Popular Posts
Topics
News
(108)
Artists
(83)
Local
(45)
Views
(41)
Music
(38)
International
(36)
Relationships
(34)
Universities
(28)
Sports
(25)
Sports Stars
(25)
Business
(14)
Life Style
(14)
Actors
(10)
OFFclass
(10)
Entrepreneur
(9)
Events
(9)
Health
(9)
Hustles
(9)
Who Hit A Lottery?
(7)
Fashion
(4)
High Schools
(4)
Movies/TV Series
(4)
Talent
(3)
Education
(1)
Tech
(1)
Archive
-
▼
2017
(182)
- November 2017 (2)
- September 2017 (20)
- August 2017 (46)
- July 2017 (6)
- June 2017 (2)
- May 2017 (1)
- April 2017 (45)
- March 2017 (51)
- February 2017 (8)
- January 2017 (1)
-
►
2016
(94)
- December 2016 (1)
- November 2016 (3)
- October 2016 (22)
- September 2016 (68)





















