Tuesday, September 6, 2016

Kuizawadia Taifa Stars Dola 10,000 Za Marekani TFF Watuma Salamu Za Shukrani Kwa Gavana Wa Nigeria Kwa

Taifa Stars ilicheza mechi hiyo Jumamosi Septemba 3, 2016 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017). Katika mchezo huo ambao mashabiki waliingia bure, Taifa Stars ilifungwa bao 1-0 mara baada ya kuibana Super Eagles hivyo kumsukuma Gavana huyo kuandaa hafla ya chakula cha jioni ambako mbali ya kuizawadia Stars, pia aliizawadia Super Eagles dola 35,000 za Marekani.

Taifa Stars ilitua Dar es Salaam usiku wa kuamkiia leo Septemba 5, 2016 ambako baadhi ya wachezaji walipelekwa Hoteli ya Urban Rose, iliyoko katikati ya Jiji la Dar es Salaam wakati wengine hususani wale wa timu ya Azam FC walichukuliwa na viongozi wao kwa ajili ya safari ya kwenda Mbeya ambako Jumatano wanatarajiwa kucheza na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaofanyika Uwanja wa Sokoine mjini humo.
Kadhalika wachezaji wa Young Africans nao walichukuliwa kwa ajili ya safari ya kwenda Mtwara ambako watakuwa na mchezoi dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini humo wakati nyota wa Simba watabaki hapa Dar es Salaam kwani Jumatano itakuwa na kibarua dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Wakati nyota 18 wakitua Dar es Salaam, Nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta aliishia Nairobi, Kenya ambako aliunganisha ndege ya kwenda Brussels, Ubelgiji.
Licha ya mchezo huo kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini ulikuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kwa fainali hizo kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.
Wachezaji waliotua ni
Makipa-
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC
Mabeki
Vicent Andrew – Young Africans
Mwinyi Haji – Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe – Azam FC
David Mwantika – Azam FC
Viungo
Himid Mao – Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi – Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania
Washambuliaji
Jamal Mnyate – Simba
Simon Msuva – Young Africans
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco – Azam FC
Mbwana Samatta –KRC Genk ya Ubelgiji
Viongozi waliofika Dar ni:
Ahmed Mgoyi – Mkuu wa msafara
Charles Boniface Mkwasa- Kocha Mkuu
Hemedi Morocco – Kocha Msaidizi
Hussein Swedi – Mtunza Vifaa
Richard Yomba – Daktari wa timu
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.