Showing posts with label Who Hit A Lottery?. Show all posts
Showing posts with label Who Hit A Lottery?. Show all posts

Tuesday, September 5, 2017

Monday, August 14, 2017

Monday, October 3, 2016

MTV MAMA; Hawa Ndio Chipukizi Wa Afrika, Ambao Raymond Atachuana Nao

Kijana wa WCB, Raymond amefanikiwa kutajwa kwenye tuzo za mwaka huu za MTV MAMA. Anawania kipengele cha msanii bora anayechipukia, wao wanakiita Best Breakthrough Act.



Anaonesha umwamba na chipukizi wengine wa Afrika. Wafahamu hapo chini pamoja na nyimbo zao.

Simi – Nigeria
Nathi – Afrika Kusini
Nasty C – Afrika Kusini
 
 Franko – Cameroon

 Falz – Nigeria
Emtee – Afrika Kusini
 
Share:

Thursday, September 29, 2016

Kevin Hart aongoza orodha ya wachekeshaji wanaolipwa zaidi duniani

Forbes wametoa orodha mpya ya wachekeshaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani. Kevin Hart ndiye anayeongoza orodha hiyo akiwa amelipwa kiasi cha $87.5 milioni kuanzia mwezi Juni mwaka mpaka kufikia Juni mwaka huu.

Nafasi hiyo kwa muda mrefu imekuwa ishikiliwa na Jerry Seinfeld ambaye kwa sasa ametupwa kwenye nafasi ya pili. Kwenye orodha hiyo pia yupo mchekeshaji wa kike, Amy Schumer.
Hii ni orodha ya wachekeshaji wengine wanaolipwa zaidi.
1) Kevin Hart ($87.5 million)
2) Jerry Seinfeld ($43.5 million)
3) Terry Fator ($21 million)
4) Amy Schumer ($17 million)
5) Jeff Dunham ($13.5 million)
6) Dave Chappelle ($13 million)
7) Jim Gaffigan ($12.5 million)
8) Gabriel Iglesias ($9.5 million)
9) Russell Peters ($9 million)
10) John Bishop ($7 million)
Share:

Tuesday, September 6, 2016

Monday, September 5, 2016

Mwasiti kufungua NGO ya mambo ya elimu

Msanii mkongwe wa muziki Mwasiti Almas ameweka wazi mpango wake wa kufungua NGO ambayo itakuwa inasaidia vijana wa kike katika ya elimu.


Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Unaniangalia’ amesema baada ya kufanya kazi ‘Sister Tanzania’ ameona vijana wengi wanakosa elimu kutokana na changamoto mbalimbali.
Share:

Hoteli Ya Kifahari Ya Arusha ‘Snow Crest’ Kupigwa Mnada, Ni Kutokana Na Kutolipa Michango Ya NSSF

Hoteli ya Kifahari ya Arusha iitwayo Snow Crest itapigwa mnada mwezi huu kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye gazeti.


Tangazo hilo lililotolewa na kampuni inayojulikana kama First World Investment Court Brokers, limedai kuwa hoteli hiyo itapigwa mnada Septemba 23, saa tano asubuhi.
Mwakilishi wa kampuni hiyo, Allan R Mollel ameiambia Bongo5 kuwa hoteli hiyo ilipelekwa mahakamani na shirika la hifadhi ya jamii, NSSF kwa kushindwa kuwalipa wafanyakazi michango yao.

“Hiyo hoteli inauzwa kwasababu ya kesi iliyokuwa mahakamani ambayo hoteli hiyo inadaiwa na NSSF michango ile ya wafanyakazi kwa maana kwamba hiyo hoteli walikuwa hawafikishi michango ya wafanyakazi NSSF. Kwahiyo NSSF wakafungua kesi wameshinda na wakaomba kuuza hii hoteli ili kuweza kupata michango hiyo ya wafanyakazi,” Mollel ameiambia Bongo5.

Amedai kuwa NSSF inaidai hoteli hiyo shilingi milioni 442 ambazo ni michango ya NSSF kwa wafanyakazi wake. Hata hivyo Mollel amesema kisheria hoteli hiyo bado ina nafasi ya kuzilipa fedha hizo kwa NSSF pamoja na gharama za dalali na wakaendelea kuwa na umiliki wa hoteli hiyo.
“Sasa hivi kilichoongezeka hapo ni gharama za dalali,” amesema.
“Kama wataweza kulipa fedha zote wanazodaiwa na NSSF, wakalipa na gharama za dalali, mambo yatakuwa yamefika mwisho.”
Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.