Cristiano Ronaldo alifunga bao lakini baadaye akafukuzwa uwanjani huku Real Madrid wakilaza Barcelona 3-1 katika Super Cup ya Uhispania, mechi ya mkondo wa kwanza.
Gerard Pique alijifunga kutoka kwa krosi ya Marcelo kabla ya Lionel Messi kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti.
Ronaldo, aliyeingia kama nguvu mpya alirejesha Real Madrid mbele alipokimbia kutoka katikati ya uwanja na kufunga.
Alipewa kadi ya njano kwa kuvua shati lake kusherehekea.
Muda mfupi baadaye, alioneshwa kadi nyingine ya manjano kwa kujiangusha na akafukuzwa uwanjani.
Marco Asensio alifunga la tatu.
Ronaldo aliamini kwamba alifaa kupewa penalti baada yake kuanguka alipokabiliwa na Samuel Umtiti, na alionekana kumsukuma refa baada yake kuoneshwa kadi nyekundu.
Ronaldo alikaa dakika 24 pekee uwanjani.
Barcelona walionekana kutatizika bila Neymar ambaye alihamia Paris Saint Germain kwa rekodi ya dunia ya £200m.
Real watakuwa wenyeji wa Barca mechi ya marudiano Jumatano saa 22:00 BST (saa sita usiku saa za Afrika Mashariki).
Barcelona walimchezesha Gerard Deulofeu safu ya mashambulizi pamoja na Lionel Messi na Luis Suarez