Monday, August 14, 2017

Neymar afunga mechi yake ya kwanza Paris St-Germain

Neymar alifunga bao mechi yake ya kwanza katika klabu yake mpya ya Paris St-Germain baada ya kununuliwa kwa rekodi ya dunia ya £200m kutokaBarcelona.

Raia huyo wa Brazil alichangia katika mabao yote matatu yaliyofungwa na PSG dhidi ya Guingamp ambao wamefanikiwa kudumisha rekodi yao ya kushinda 100% mwanzo wa msimu.
Jordan Ikoko alifungua ukurasa wa mabao kwa kujifunga baada ya pasi ya Neymar kwa Edinson Cavani kuzimwa
Neymar kisha alimsaidia Cavani kufunga kwa pasi safi kabla ya nyota huyo wa uruguay naye kumpa pasi Neymar ambaye alifunga dakika za mwishomwisho akiwa hatua sita hivi kutoka kwenye lango.
Mchezaji huyo wa Brazil mwenye miaka 25 alichezeshwa upande wa kushoto lakini alihusika kati safu ya mashambulizi.
Alitamba sana uwanjani kwa kugeresha na kushambulia, ingawa mengi ya makombora yake yalizimwa kabla yake kufanikiwa kufunga dakika za mwisho.
Neymar kwa takwimu
Akilinganishwa na washambuliaji wenzake Edinson Cavani na Angel di Maria
Makombora6pamoja na yaliyozimwa(sawa na Cavani na Di Maria)
Pasi88 (Cavani 21, Di Maria 63)
Ufasaha wa pasi76% (Cavani 91%, Di Maria 86%)
Pasi muhimu7 (Cavani 2, Di Maria 0)
Kukabili wapinzani22 (Cavani 4, Di Maria 7)
Kufanikiwa kukabili wapinzani 73% (Cavani 50%, Di Maria 29%)
Kupoteza mpira 33 (Cavani 6, Di Maria 13)

Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.