Showing posts with label Sports Stars. Show all posts
Showing posts with label Sports Stars. Show all posts

Monday, September 25, 2017

Sunday, September 24, 2017

Kwa sasa Cesar Azpillicueta na Alvaro Morata ndio combination hatari kuliko yoyote barani Ulaya


Hii leo mtaani mashabiki wa Chelsea wanatembea vifua mbele baada ya hapo jana Alvaro Morata kuionesha dunia ni nini amekuja kufanya Uingereza na kuwanyamazisha waliokuwa wanamsema.

Tayari Conte amemwagia sifa nyingi mshambuliaji huyo na kusema kwamba ni kijana mzuri sana kiasi kwamba hata kama una binti unataka muoezesha baasi muozeshe kwa Alvaro, lakini kuna mambo yafuatayo ya kufahamu kutokana na ushindi wa jana wa Chelsea.

Alvaro Morata alifunga hat trick yake ya kwanza, lakini je unajua ya kwamba hat trick hii ya Morata imechukua muda mrefu tofauti na Diego Costa. Diego Costa yeye alitumia mechi 4 tu kufunga hat trick huku Morata akitumia 6.

Wakati Morata akifanya hivyo, mchezaji mwingine mpya Chelsea Tiemoue Bakayoko yeye kwa siku ya jana alifanya tackle zilizofanikiwa 5, hiyo ni idadi ambayo jana katika michezo yote hakuna kiungo aliyemzida kwa tackling.

Chelsea hapo hapo, baada ya magoli matatu ya jana ya Morata inawafanya Chelsea kwa sasa mabao 10 kati ya 13 waliyofunga msimu huu yamefungwa na watu wa taifa moja la Hisapania.

Lakini vile vile kama hujui tu ni kwamba katika ligi 4 kubwa barani Ulaya hakuna Combination ambayo imezalisha mabao mengi hadi sasa kama combination ya Alvaro Morata na Cesar Azipiculeta, hadi sasa wametengeneza mabao manne.
Share:

Friday, August 18, 2017

Tuesday, August 15, 2017

Monday, August 14, 2017

Sunday, July 9, 2017

Friday, April 14, 2017

Tuesday, April 11, 2017

MICHEZO BAD NEWS: RFEF imemfungia Neymar leo April 11 2017

Staa wa soka wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Neymar amekutana na adhabu ya kufungiwa mechi 3 kuichezea FC Barcelona na shirikisho la soka Hispania ( Royal Spanish Football Federation (RFEF) kwa makosa mawili.
Neymar amefungiwa mechi tatu, mechi moja ni kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano wakati wa mchezo dhidi ya Malaga uliyomalizika kwa FC Barcelona kupoteza kwa magoli mawili kwa 2-0 lakini mechi ya mbili kwa kosa la kumpongeza kwa kejeli fourth official wakati anatoka nje ya uwanja.
Neymar alipooneshwa kadi ya pili ya njano
Mchezaji huyo raia wa Brazil alitoa lugha za kejeli kwa fourth official wakati anatoka uwanjani kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano, refa wa game hiyo Jesus Gil Manzano ndio aliandika ripoti hiyo, Neymar sasa atakosa mchezo dhidi ya Real SociedadReal Madrid naOsasuna.
Share:

“Demu” Wa Ronaldo Aondolewa Kazini Kwa Sababu Ya Bwana Ake.


Kimwana wa Cristiano Ronaldo imemlazimu kuachana na kazi yake ambapo alikuwa ni meneja mauzo katika kampuni ya Prada.
Georgina Rodriguez ambaye alikuwa anapokea kiasi kinachokaribia paundi £1,370 kwa mwezi kwa kamisheni pekee kila mwezi ameamua kuondoka kwenye kiti chake hizo kutokana na rundo la waandishi wanaofika hapo kila mara jijini Madrid wakiajribu kukutana naye na kusaka taarifa mbalimbali
Ripoti iliyotolewa na jarida la El Mundo linasema kuwa hali ilikuwa mbaya na ambayo haikuwa na faida kwa baadae na kibiashara kutokana na suala hilo kuwa nje ya uwezo
Baadhi wa waandishi walifikia hatua ya kujifanya wateja ili tu wapate taarifa za Rodriguez ambazo wangeweza kuziandika ama kuziripoti.
Baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili na mabosi wake, binti huyo mwenye umri wa miaka 22 ilimbidi kuachia nafasi yake.
Na kazi ya Prada haikuwa ya kwanza kwenye suala la mitindo ambalo Rodriguez amejikita ambayo kapoteza kwani kutokana na mahusiano yake na Cristiano Ronaldo ilibidi aache kazi kwenye kampuni ya Gucci.
Aliondolewa na uongozi wa Gucci mwisho wa mwezi November, huku mabosi wakihofia kuwa wingi na uwepo wa waandishi kila mara ungeathiri mahusiano yao na wadau wao na wahisani.
Share:

Friday, April 7, 2017

Thursday, April 6, 2017

Saturday, March 25, 2017

Mbwana Samatta Anamiliki Mijengo Sita Dar

Achana na uwezo wa Mbwana Samatta akiwa uwanjani. Mchezaji huyo siyo wa mchezo pia kiuchumi– ana mijengo takribani sita jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti, mshambuliaji huyo wa Taifa Stars na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amewekeza zaidi katika kujenga nyumba ambazo zote hizo zipo Mbagala lakini katika maeneo tofauti tofauti.
Imedaiwa kuwa mijengo hiyo ya Samatta ipo Majimatitu, Kiburugwa Shimo la Mchanga, Mbande na Mbagala Saku (zote zipo Mbagala) ukiachana na ile ikulu yake anayoijenga huko kibada ambayo tayari imeisha japo kuna marekebisho madogo madogo yanaendelea.
Wakati huo huo rafiki wa karibu wa mchezaji huyo aliliambia gazeti hilo kuwa mchechezaji huyo anaishi katika nyumba yake aliyopanga (Apartment) iliyopo katika ufukwe wa bahari ya Hindi maeneo ya Kijichi.
“Anapokuja kwa mapumziko kwao huwa anakwenda kwa sababu ni nyumbani kwa ajili ya kusalimia na mambo mengine lakini hakai hapo, anaishi Kijichi kuna nyumba nzuri ya kifahari ipo ufukweni mwa bahari amepanga,”alisema.
Share:

Monday, October 10, 2016

CAF kuja kukagua uwanja wa CCM Kirumba

Wataalamu wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), wanatarajiwa kutua nchini wakati wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kukagua Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Huu ni utaratibu wa CAF ambako baada ya muda hutembelea nchi wanachama kuangalia maendeleo ya miundombinu ya mpira wa miguu kabla ya kupandisha hadhi ya viwanja kwa ajili ya michuano ya kimataifa inayosimamiwa na kuendeshwa na CECAFA, CAF na FIFA.
Ukaguzi huo unafanyika wakati Tanzania inasubiri majibu ya Uwanja wa Sokoine wa Mbeya ambao ulikwiisha kukaguliwa na mapendekezo ya uboreshwaji kutolewa ili uweze kupandishwa hadhi ya matumizi ya kuchezwa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani, michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA.
Viwanja ambavyo CAF na FIFA inavitambua nchini Tanzania hadi sasa ni Amani wa Unguja, Zanzibar; Kaitaba wa Kagera, Azam Complex na Uwanja Mkuu wa Taifa vya Dar es Salaam.
Endapo CCM Kirumba utapitishwa, kutakuwa na nafasi ya kuruhusu kuchezwa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA.
Kirumba inaingia kwenye orodha ya viwanja vya Gombani ulioko Pemba; Sokoine wa Mbeya, Kaitaba wa Kagera ambavyo vilikwisha kukaguliwa na sasa vinasubiri kupitishwa ili kutumika kimataifa. Ujio wa viwanja hivyo, utapanua wigo wa Tanzania kuandaa michuano mikubwa katika ngazi ya timu za taifa kimataifa
Share:

Tuesday, September 20, 2016

Serengeti Boys kuweka kambi nje nchi

Baada ya kuifunga Congo-Brazzaville mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika, timu ya taifa ya vijana, Serengeti inatarajiwa kuondoka Alhamis wiki hii kwenda kupiga kambi nje ya nchi.


Hata hivyo, taratibu zinapangwa kuhakikisha kwamba timu hiyo inakwenda kupiga kambi kwenye nchi tulivu inayolingana hali ya hewa na Congo Brazzaville kadhalika chakula pamoja na mazingira.
Tanzania na Congo Brazzavile, zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo Brazzaville na timu itakayopata ushindi wa jumla katika michezo miwili itafuzu kwa fainali hizo.
Katika mchezo uliofanyika Septemba 18, Serengeti Boys ilipata mabao yake kupitia Yohana Mkomola na Abdi Makamba wakati yale ya Congo yalifungwa na Langa-Lesse Percy na Makouana Beni ambao mashabiki wa soka walikuwa wakiwalalamikia kuwa ni “wakubwa.”
Ili ifuzu kwa fainali zitakazofanyika mwakani huko Antananarivo, Madagascar katika fainali zitakazoanzia Aprili, 2017, Serengeti Boys inatakiwa ibaki na matokeo yake ya sasa na ihakikishe inapata ushindi na kama sare basi wapate bao kufuta faida ya bao la ugenini ambalo Congo Brazzaville walikuwa wanasheherekea baada ya mchezo.
Share:

Monday, September 19, 2016

Pogba awapa moyo mashabiki wake wa Manchester United

Mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa Paul Pogba wa Manchester United amelazimika kuwapa moyo mashabiki wake baada ya timu yake kupoteza mechi mbili mfululizo








Jumapili, Septemba 18 ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa tano wa ligi kuu ya England dhidi ya Watford na kufungwa magoli 3-1. Kiungo huyo wa Ufaransa ambaye hadi kwa sasa hajafanya vizuri kama wengi walivyokuwa wana matarajio akiwa na Man United toka avunje rekodi ya usajili.
Kupitia Instagram, Pogba ameandika: Asante kwa mashabiki wote kuwa pamoja na sisi matokeo bado sio mazuri kwa upande wetu, lakini tunaendelea kupambana, Man United tunaweza.”

Share:

Tuesday, September 6, 2016

Mkhitaryan Hana Uhakika Kama Atacheza Derby

Kiungo wa Manchester United na timu ya Taifa ya Armenia Henrikh Mkhitaryan hana uhakika kama atacheza Manchester Derby baada kuumia katika mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Czech jumatano iliyopita.

Henrikh Mkhitaryan kupitia akaunt yake ya twitter alipost ujumbe huu

Not sure yet if I’ll bit fit for the derby, but I’m motivated as ever to put all energy to be in great shape asap!!
Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.