Tuesday, April 11, 2017

“Demu” Wa Ronaldo Aondolewa Kazini Kwa Sababu Ya Bwana Ake.


Kimwana wa Cristiano Ronaldo imemlazimu kuachana na kazi yake ambapo alikuwa ni meneja mauzo katika kampuni ya Prada.
Georgina Rodriguez ambaye alikuwa anapokea kiasi kinachokaribia paundi £1,370 kwa mwezi kwa kamisheni pekee kila mwezi ameamua kuondoka kwenye kiti chake hizo kutokana na rundo la waandishi wanaofika hapo kila mara jijini Madrid wakiajribu kukutana naye na kusaka taarifa mbalimbali
Ripoti iliyotolewa na jarida la El Mundo linasema kuwa hali ilikuwa mbaya na ambayo haikuwa na faida kwa baadae na kibiashara kutokana na suala hilo kuwa nje ya uwezo
Baadhi wa waandishi walifikia hatua ya kujifanya wateja ili tu wapate taarifa za Rodriguez ambazo wangeweza kuziandika ama kuziripoti.
Baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili na mabosi wake, binti huyo mwenye umri wa miaka 22 ilimbidi kuachia nafasi yake.
Na kazi ya Prada haikuwa ya kwanza kwenye suala la mitindo ambalo Rodriguez amejikita ambayo kapoteza kwani kutokana na mahusiano yake na Cristiano Ronaldo ilibidi aache kazi kwenye kampuni ya Gucci.
Aliondolewa na uongozi wa Gucci mwisho wa mwezi November, huku mabosi wakihofia kuwa wingi na uwepo wa waandishi kila mara ungeathiri mahusiano yao na wadau wao na wahisani.
Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.