Thursday, April 6, 2017

Swali walilouliza Europa League kuhusu Mbwana Samatta leo

Tukiwa tunaelekea kutazama michezo ya kwanza ya robo fainali
ya UEFA Europa Leaguealhamisi ya April 13 2017, jina la mtanzania Mbwana Samatta limezidi kuchukua headlines katika michuano hiyo, Samatta na timu yake ya KRC Genk watacheza mchezo wao wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Celta Vigo ya Hispania.


Leo kupitia ukurasa rasmi wa twitter account ya UEFA Europa League wamelitaja jina la mtanzania Mbwana Samatta kwa kumpost katika twitter account yao na kuuliza swali je huyu ni wa kumuangalia?hiyo ni baada ya Samatta kuonesha uwezo mkubwa akiwa naGenk katika mechi 5 zilizopita.


Samatta katika mechi tano zilizopita za KRC Genk za mashindano tofauti amefanikiwa kufunga jumla ya goli 6 hivyo Samatta kwa takwimu hizo anatajwa kama mchezaji wa kuangaliwa, Genk watacheza mchezo wao wa kwanza wa Europa League ugenini dhidi yaCelta Vigo nchini Hispania katika uwanja wa Balaidos saa 22:05 kwa saa za Afrika Mashariki.

Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.