Monday, August 14, 2017

Zinedine Zidane: Mkufunzi mkuu wa Real Madrid kutia saini mkataba mpya

Mkufunzi mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane ameafikiana na mabingwa hao wa Ulaya na Uhispania kuhusu mkataba mpya wa miaka mitatu.

Kiungo huyo wa kati wa zamani wa Real, katika katika miezi 18 ambayo amekuwa kwenye usukani, ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili na taji la La Liga mara mbili.
Akiongea mkesha wa mechi ya kwanza ya mkondo wa kwanza ya Super Cup ya Uhispania itakayochezewa Barcelona, alisema: "Hadithi yangu na Real Madrid ni zaidi ya mikataba na saini.
"Nina furaha kubwa kuhusishwa na klabu hii. Lakini mkatana hauna maana yoyote."
Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye miaka 45 alikuwa mkufunzi wa Timu B ya Real kabla ya kuchukua nafasi ya Rafael Benitez Januari 2016.
Aliongeza: "Unaweza kutia saini mkataba wa miaka 10, 20. Najua niko wapi na nataka kufanya nini.
"Katika mwaka mmoja, pengine sitakuwa hapa. Mimi na Real Madrid hatutajibizana, daima.."
Real watacheza dhidi ya Barca Jumapili mechi itakayoanza saa 21:00 BST (saa tano usiku Afrika Mashariki). Mechi ya marudiano itachezewa Bernabeu Jumatano saa 22:00 BST (Saa sita Afrika Mashariki).
Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.