Meneja wa Chelsea Antonio Conte anasema hana wasi wasi kufuatia kushindwa kwa klabu hiyo kuwasainia wachezaji wapya msimu huu.
Chelsea imewasaini wachezaji wanne kwa jumla ya pauni 129, lakini wacheza wengi walikihama klabu hiyo wakiwemo John Terry na Nemanja Matic.
Msimu wao ulianza kwa kipigo cha nyumbani Chelsea waliposhindwa mabao 3-2 na Burnley siku ya Jumamosi katika mechi ambayo Gary Cahill na Cesc Fabregas walitumuliwa uwanjani.
"Klabu kinajaribu kufanya kila kiwezalo," alisema Conte.
Sawa na mlinzi John Terry na mchezaji wa kiungo cha kati Matic, Chelsea wamemuuza Amir Begovic kwenda Bournmouth huku mfungaji bora wa msimu uliopita Diego Costa ameambiwa kuwa yuko huru kuondoka klabu hiyo.
Kusainiwa kwa mchezaji wa kiungo cha kati Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco, mshambuliaji Alvaro Morata kutoka Real Madrid, mlinzi Antonio Rudiger kutoka Roma na aliyekuwa kipa wa Manchester City Willy Caballero, kujaza pendo lililoachwa wazi.
Hata hivyo Conte ameweka wazi mipango yake ya kusaini wachezaji zaidi ili kuboresha kikosi chake kwa msimu huu.