Saturday, March 25, 2017

Mbwana Samatta Anamiliki Mijengo Sita Dar

Achana na uwezo wa Mbwana Samatta akiwa uwanjani. Mchezaji huyo siyo wa mchezo pia kiuchumi– ana mijengo takribani sita jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti, mshambuliaji huyo wa Taifa Stars na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amewekeza zaidi katika kujenga nyumba ambazo zote hizo zipo Mbagala lakini katika maeneo tofauti tofauti.
Imedaiwa kuwa mijengo hiyo ya Samatta ipo Majimatitu, Kiburugwa Shimo la Mchanga, Mbande na Mbagala Saku (zote zipo Mbagala) ukiachana na ile ikulu yake anayoijenga huko kibada ambayo tayari imeisha japo kuna marekebisho madogo madogo yanaendelea.
Wakati huo huo rafiki wa karibu wa mchezaji huyo aliliambia gazeti hilo kuwa mchechezaji huyo anaishi katika nyumba yake aliyopanga (Apartment) iliyopo katika ufukwe wa bahari ya Hindi maeneo ya Kijichi.
“Anapokuja kwa mapumziko kwao huwa anakwenda kwa sababu ni nyumbani kwa ajili ya kusalimia na mambo mengine lakini hakai hapo, anaishi Kijichi kuna nyumba nzuri ya kifahari ipo ufukweni mwa bahari amepanga,”alisema.
Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.