Monday, September 5, 2016

Mwasiti kufungua NGO ya mambo ya elimu

Msanii mkongwe wa muziki Mwasiti Almas ameweka wazi mpango wake wa kufungua NGO ambayo itakuwa inasaidia vijana wa kike katika ya elimu.


Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Unaniangalia’ amesema baada ya kufanya kazi ‘Sister Tanzania’ ameona vijana wengi wanakosa elimu kutokana na changamoto mbalimbali.


“Ili kudhibitisha kwamba napenda kujitolea kwa jamii katika siku za hivi karibuni natarajia kufungua NGO ya mambo ya elimu na ninaamini nitaifikia namba kubwa ya vijana wa Tanzania,” Mwasiti aliliambia gazeti la Mtanzania.
 “Lengo langu ni kuwatoa vijana sehemu moja na kuwapeleka nyingine kupitia elimu itakayokuwa naitoa maana wapo watu wanatamani kufika mahali nilipo lakini hawajui namna ya kufika… hii haitakuwa mara yangu ya kwanza kwa sababu nimefanya kazi na Sister Tanzania na nimepata uzoefu wa kutosha. Mfano kuna mambo ambayo kama msanii nikimwambia mtoto inakuwa rahisi kutekeleza kuliko akiambiwa na wazazi wake.”

Muimbaji huyo alisema atadili na wanawake wenzake, kwasababu kwake inakuwa rahisi zaidi kutoa elimu.
Alisema alipenda iwe kwa wanaume pia lakini atashindwa kwa kuwa kuna mambo atashindwa kuyazungumza na watoto wa kiume kutokana na utofauti wa kijinsia.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.