Wito huo umetolewa na mratibu wa midahalo hiyo inayorushwa kupitia runinga ya Channel 10,Shukuru Ngongoje. Amesema nia ya midahalo hiyo ni kuwasaidia wanafunzi katika uelewa wa kujiendeleza mbele na mustakabali mzima wa masomo.
“Nichukue fursa hii sasa kuweza kutoa wito kwa shule mbalimbali za serikali na shule za watu binafsi kwaajili ya kuweza kushiriki mashindano haya ya debate,” alisema.
Aliongezea kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya maonesho ya saba saba na kwamba maandalizi yamekamilika.
“Tunawasihi wamiliki wa shule mbalimbali kuweza kujitokeza na kushiriki,” alisisitiza Ngongoje.
BY: EMMY MWAIPOPO
0 comments:
Post a Comment