Thursday, September 29, 2016

Kevin Hart aongoza orodha ya wachekeshaji wanaolipwa zaidi duniani

Forbes wametoa orodha mpya ya wachekeshaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani. Kevin Hart ndiye anayeongoza orodha hiyo akiwa amelipwa kiasi cha $87.5 milioni kuanzia mwezi Juni mwaka mpaka kufikia Juni mwaka huu.

Nafasi hiyo kwa muda mrefu imekuwa ishikiliwa na Jerry Seinfeld ambaye kwa sasa ametupwa kwenye nafasi ya pili. Kwenye orodha hiyo pia yupo mchekeshaji wa kike, Amy Schumer.
Hii ni orodha ya wachekeshaji wengine wanaolipwa zaidi.
1) Kevin Hart ($87.5 million)
2) Jerry Seinfeld ($43.5 million)
3) Terry Fator ($21 million)
4) Amy Schumer ($17 million)
5) Jeff Dunham ($13.5 million)
6) Dave Chappelle ($13 million)
7) Jim Gaffigan ($12.5 million)
8) Gabriel Iglesias ($9.5 million)
9) Russell Peters ($9 million)
10) John Bishop ($7 million)
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.