Tuesday, September 5, 2017

Tiwa Savage ampagawisha Jay Z kwa show kali

First lady wa Mavin Record , Tiwa Savage ameamsha shangwe kutoka kwa mashabiki lukuki  waliokuwepo katika tamasha la Made in America Festival 2017, liliofanyika katika uwanja wa Benjamin Franklin Parkway nchini Ufaransa hapo jana(Jumapili).

Tamasha hili lililokuwa likifanyika kwa siku
mbili mfululizo, ambapo siku ya jana mrembo huyo alipata nafasi ya kukonga nyoyo za mashabiki wake. Kwa muda kadhaa kumekuwa na tetesi kuwa mrembo huyo anaweza akasajiliwa katika lebo ya Roc Nation, inayomilikiwa na rapper Jay Z ambaye naye alikuwepo katika tamasha hilo na alimpongeza mwanadada huyo kwa kupiga show kali.





Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.