Monday, September 5, 2016

Exclusive: Sikiliza wimbo wa Vanessa na Jux uliowakutanisha mara ya kwanza kabla hawaja na uhusiano

Hapo zamani za kale, Vanessa Mdee alikuwa na maisha yake, na Jux pia aliwa na maisha yake lakini muziki ulikuja kuwakutanisha na hadi leo imebaki story.
Katika kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake [Jux] iliyokuwa Alhamis hii, Vee Money ameamua kuwaonjesha wimbo uliowakutanisha studio kwa mara ya kwanza na Jux. Walikutana kwenye studio za B’Hits zaidi ya miaka miwili iliyopita na Jux kumuomba Vanessa aweke verse yake kwenye wimbo huo.

“Your boy asked me if I would spit some bars on your song. I said no. Then walked into the studio and met you and instantly had a change of heart,” ameandika Vanessa kwenye post ya kumpongeza Jux.
Na kweli, Vee alitupia mistari mikali ya hip hop na kudhirihisha kuwa ni muimbaji mwenye vipaji vingi.
Sikiliza kipande cha Vanessa hapo chini



Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.