Tuesday, September 6, 2016

Joh Makini na msanii wa Nigeria, Falz kuungana kwenye Coke Studio Africa msimu wa 4

Msanii wa Hip Hop Bongo, Joh Makini yupo nchini Nairobi, Kenya akiwa ni miongoni mwa wasanii wanne watakaoiwakilisha Tanzania kwenye kipindi cha Coke Studio Africa Season 4.


Huu ni msimu wa pili kwa rapper huyo wa Bongo kushiriki kwenye kipindi hicho. Kwa msimu wa tatu, Joh Makini aliungana na msanii wa Nigeria, Chidinma ambaye walitengeneza mchanganyiko uliowavutia mashabiki wa kipindi hicho kitu kilichopelekea mpaka wakafanya collabo ya wimbo wa ‘Perfect Combo’.


Kwa msimu huu Joh Makini ameungana na rapper wa Nigeria, Falz ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Chardonnay Music’ lakini ikiwa ni msimu wake wa kwanza kushiriki kwenye kipindi hicho.

Huu ni wimbo wa Falz, ‘Chardonnay Music’ ambao ameuachia wiki iliyopita.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.