Msanii wa muziki Jux amesema mwonekano mzuri kwa msanii ni kitu muhimu ambacho kinamjenga msanii kujiamini pamoja na kuwa tofauti na wale anaowapa huduma
Akiongea na Clouds TV wiki hii, Jux amesema hapendi kuona msanii anashindwa kujali mwonekano wake.
“Sometime hata mimi mwenyewe sipendi kuona mtu au msanii kila siku yupo vile vile,” alisema Jux. “Kama msanii lazima ubadilike, hata mimi huwaga nikipost picha najiangalia naona hapa natakiwa kubadilika, hivi nimeshazoeleka,”
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na brand yake ya ‘African Boy’, amewataka wasanii wenzake kuhakikisha wanajiweka vizuri katika mwonekano.
0 comments:
Post a Comment