Monday, September 5, 2016

Mr Blue Kumpeleka Mahakamani Anayejaribu Kuharibu Ndoa Yake

Mkali wa wimbo ‘Mboga Saba’ Mr Blue ambaye  hivi karibuni alipatwa na msukosuko wa kuyumba kwa ndoa yake, kutokana na kusambaa kwa tetesi za kuwasiliana na ex wake Najma, amesema yuko tayari kumchukulia hatua za kisheria aliyesababisha ugomvi huo.



Rapper huyo amesema yeye binafsi hakuwasiliana na Naj, isipokuwa habari hizo zilipoanza alidhani ni kiki inayotengenezwa na Naj pamoja nampenzi wake Barakah The Prince, ili kuachia wimbo wao wa pamoja.
“Ile habari ilikuwa ya uongo, mwanzoni mi nilihisi Barakah na mchumba wake Najma watakuwa wameitengeneza kwa ajili ya mambo yao ya kutafuta kiki, kwa sababu ilisemekana kuna nyimbo yao wanataka kutoa Barakah na Najma, kwa hiyo wanatafuta kama kiki kutumia ubavu wangu, nikabahatika kukutana na Barakah na kumshika mkono, na kumwambia akubali mbele za watu, akasema hajui hiyo taarifa”, Mr Blue alikiambia kipindi cha Planet Bongo.

Aliongeza,”Hatua za kisheria lazima zichukuliwe unajua hivi vitu sio vitu vya kuharibiana, mi sa hivi nishakuwa mtu mzima, siwezi kurudia matapishi ambayo nishawahi kuyatapika, eti nikampigie Najma sijui niwe naye, kwa sababu mimi najua mke wa kumuoa najua mwanamke wa kuwa naye ndio maana nikamchagua mke wangu, na nampenda na amenizalia watoto wazuri, kwa hiyo siwezi tena kufikiria eti kumpigia Najma, siwezi kufikiria kugombana na Barakah The Prince, kwanza hatulingani, mi wakati naanza mziki ye bado yuko shule anasoma, kama ni kweli ni wao japokuwa Barakah amenithibitishia sio wao, nikijua ni wao lazima nitafute njia ya kuwashikisha adabu.”
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.