Wanafunzi nchini wametakiwa kujikita zaidi katika masomo yao na kujiepusha kujiingiza katika makundi hatarishi yanayoweza kuwapelekea kujihusisha na matumizi ya maadwaya ya kulevya.
Akitoa elimu ya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanafunzi wa skuli ya Sekondari BUBUBU msaidizi mkaguzi kitengo cha upepelezi kituo cha polisi Bububu Jongo Ali Jongo amesema kujiingiza kwa matumizi ya madawa ya kulevya yataweza kuwapelekea kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji.
Nae Koplo Khamis Muhammed Rashid wa kitengo cha upelelezi Bububu amewataka wanafunzi kuwa tayari kuvifichua vitendo vyote vya udhalilishaji wa kijinsia kwa kuwa tayari kutoa ushahidi katika vyombo vya sheria.
Na;Fat hiya sheheZanzibar24
0 comments:
Post a Comment