Aika na Nahreel wana miaka minane sasa tangu waanzishe uhusiano wao uliopelekea kuzaliwa kwa kundi lao, Navy Kenzo.
Wakiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, wawili hao wamesema tangu wameanza uhusiano wao wamejiwekea desturi ya kuaminiana kiasi ambacho kila mmoja anaweza kutumia simu ya mwenzake.
Walizungumzia pia kutajwa kuwania tuzo za MTV MAMA na kuwaomba Watanzania wawapigie kura. Pia wamezungumzia jinsi ambavyo wameahirisha mara mbili kufanya video ya wimbo waliomshirikisha Alikiba kutokana na msanii huyo kubanwa na ratiba zingine.
Wamesema wataangalia iwapo watatumia muda watakaokuwa kwenye MTV MAMA wikiendi hii kukamilisha mradi huo.
0 comments:
Post a Comment