Baada ya kuwekwa jiwe la msingi
kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara za juu (interchange) katika eneo la
Ubungo jijini Dar es Salaam March 20, 2017 kwa ufadhili wa Bank ya Dunia, Rais
wa Bank hiyo Jim Yong Kim ameandika haya kuhusu jiji la Dar es Salaam na
Tanzania kwa jumla.
“Kama ilivyo miji mingi ya
Afrika, Dar es Salaam uliopo Tanzania unakua kwa haraka – na hivyo ni mji wenye
msongamano wa magari. Suluhisho linahitajika, hivyo nilipewa heshima kujumuika
na Rais John Pombe Magufuli kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya barabara ya juu
Ubungo.
‘Sehemu hii ya miundombinu
itawaunganisha watu wengi kwenye kazi na nafasi mbalimbali na kufanya safari
kwa mabasi mapya ya mwendokasi. BRT imeelezwa kuwa tayari imepunguza muda wa
kusafiri kwa dakika 90. Bank ya Dunia inafurahi kuunga mkono kazi zote na
inaangalia mbele kusaidia kulifukia pengo la miundombinu Tanzania na kwingineko
Afrika.”– Jim Yong Kim.
0 comments:
Post a Comment