Friday, March 24, 2017

Rais Magufuli Baada Ya Kufanya Ziara Ya Kushitukiza Bandari DSM Amekuta Haya


Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli alhamisi ya March 23 2017 amefanya ziara ya kushitukiza katika bandari ya Dar es Salaam, Rais amefanya ziara hiyo akiwa na lengo la kuthibitisha kama maagizo yake ya kusimamia na kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia.

Katika ziara hiyo Rais Magufuli ameshuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya March 2 2017.

Hata hivyo Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP – Ernest Mangu na vyombo vingine vya usalama kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo mpaka hapo uchunguzi wa utakapofanyika kubaini ukweli.

Pamoja na hayo Rais Magufuli ameona udanganyifu wa baadhi ya wafanyabiashara ambao wameingiza makontena huku nyaraka zikiandika kuwa yamebeba mitumba lakini yalipofunguliwa yalionekana yamebeba magari ya kifahari.

“Nataka niwaambie nchi yetu inachezewa mno, nimekuja kuyaona haya makontena kama yapo na kweli nimeyaona, sasa utaratibu utakapokamilika nataka Watanzania na dunia nzima ione kilichomo ndani kama ni mchanga kweli ama dhahabu” ~Rais Magufuli.

Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.