Thursday, April 6, 2017

Bongo Movie Yatua Kwa RC Makonda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda amepiga marufuku kuanzia Alhamisi hii tarehe 06 Aprili, 2017 uuzwaji, uingizwaji wa filamu za nje ambazo hazina stika za TRA ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha amesema baada ya siku kumi ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum wataendesha msako wa kuwakamata wote watakaokuwa wamekiuka agizo hilo.
Amesema hayo amapema leo ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya kutembelewa na wasanii wa filamu wakiongozwa na Jacob Stephan wakilalamikia kuzagaa kwa kazi zao ambazo zimedurufiwa na wafanyabishara wasiowaaminifu.
Akiongea na waandishi pamoja na wasanii hao, Mh Makonda aliwaagiza watu wa bodi ya filamu kufanya tadhmini ya haraka kubaini ni maduka mangapi yanayouza mikanda ya filamu jiji Dar es Salaam.
Wasanii hao pamoja na wasambazaji walidai hawanufaiki na kazi zao za filamu kutokana na kuwepo kwa maharamia wanaoziiba kazi hizo kwa kuzi-download kisha kuzisambaza kimagendo kwa bei ya kutupa bila ridha yao na zikiwa hazina stempu ya mamlaka ya mapato.
Wasanii wengine ambao walifika ofisini hapo ni pamoja na Ray Kigosi, Odama, Tino, Jimmy Mafufu pamoja na wasambazaji wa filamu.
Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.