Bila shaka itakuwa ni ngoma yenye histori kubwa kwa kipindi chote ndani ya Bongo Flava, lakini je hilo litatokea lini?.
Hilo ni swali ambalo hata rais wa label hiyo Diamond anajiuliza pamoja na mshabiki wao. Kupitia mtandao wa instagram Diamond ameandika, “Ushawahi waza WCB Wasafi wote kwenye ngoma moja…?
Swali hilo huwenda linaashiria kuwa siku za hivi karibuni WCB watakuja na ngoma ya pamoja.
Ndani ya WCB Diamond ameshatoa ngoma na Harmonize, Rich Mavoko, Rayvanny wakati Queen Darleen akitoa na Rayvanny, huku Rich Mavoko akitoa na Harmonize.
Mashabiki wa muziki wanaisubiria kwa hamu kolabo hiyo kama ikitokea.