Thursday, September 29, 2016

Diva: Mastaa wa Bongo waelewe thamani yao, mimi nachaji milioni 3.5 kwa appearance tu

Mtangazaji wa Clouds FM, Diva The Bawse amewataka mastaa wa Tanzania kutambua thamani ya brand zao na kuacha kujichukulia poa.
Amedai kuwa mastaa wengi wamekuwa wakitumika bure kufaidisha watu wengine na anadhani ni muhimu wakaacha kujishusha kiasi hicho.
Anadai kwa upande wake yeye, hafanyi kitu bure na kudai kuwa hata kuonekana kwenye saa moja kwenye party ya mtu, ni lazima awe amemlipa.
“My standard rate is 3.5 million in one night that including 30 minutes hosting, na sikai less than hour naondoka,” Diva ameandika kwenye blog yake.
“Ifike stage celebs wajue value yao na sio kutumika tu kwa faida ya watu wengine. Chochote unaona pia napost kwenye account zangu za mitandao kinalipiwa., lazima ujue kama wewe ni maarufu lazima ulipwe hata kutweet brand ya mtu mwingine,” ameongeza.
Mtangazaji huyo ana zaidi ya followers milioni 1.1 kwenye Instagram na amekuwa akiingiza mkwanja mrefu kwa kupost matangazo mbalimbali
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.