Kampuni inayoongoza kwa mauzo ya simu Afrika, Tecno Mobile imezindua simu mbili matata za Phantom 6 na Phantom 6 Plus katika tukio lililohudhuriwa na watu maarufu kibao katika hoteli ya Armani ambayo ipo katika jengo refu zaidi duniani Burj Khalifa.
Uzinduzi huu umefanyika wakati ambapo kampuni ya Tecno inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.
ANGALIA KIPANDE KIFUPI CHA VIDEO YA TECNO PHANTOM 6
Uzinduzi huu umefanyika wakati ambapo kampuni ya Tecno inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.
ANGALIA KIPANDE KIFUPI CHA VIDEO YA TECNO PHANTOM 6
“Imetuchukua takribani miaka 3 katika matengenezo yake na imehusisha zaidi ya wahandisi laki 5,” alisema Mkuu wa Masoko wa Tecno, Vane Ni.
“TECNO Phantom 6 inawapa watumiaji wa simu za mkononi utulivu bora pindi wanapotumia, kasi na kamera bora na nzuri ili kufurahia zaidi simu ya mkononi,” alisema Naibu Kiongozi wa Masoko wa Tecno Nigeria, Attai Oguche.
Uzinduzi ulifana sana ambapo kulikuwa na zaidi ya vyombo vya habari 70 tofauti kutoka nchi mbalimbali duniani kote na miongoni mwa mastaa waliohudhuria ni mwanamuziki mahiri wa Tanzania, Alikiba na mwanahabari ‘Mtuwa Nguvu’ Millard Ayo ambaye alishinda safari ya kwenda China.
Mwanamuziki wa kimataifa wa Tanzania, Alikiba akiwa na kifaa kipya cha Phantom 6 akifanya mauzungumzo
Baada ya uzinduzi huo Tecno Tanzania ikatangaza kwamba Phantom 6 na Phantom 6+ zitaanza kupatikana rasmi kuanzia tarehe 8 Oktoba 2016 katika duka la Tecno lililopo City Mall Posta ambapo wateja wote watakaonunua Phantom 6 siku hiyo watapatiwa vifurushi vya zawadi na kutakuwa na zawadi kubwa nono.
Pia wakatangaza kwamba kuanzia Jumatatu tarehe 3 Oktoba wateja watajaza fomu maalum ili kuweka oda zao na watazawadiwa zawadi mbalimbali zikiwemo T-Shirts, mabegi, T-Band na Sefie stick siku ya kuanza mauzo hiyo tarehe 8 Oktoba.
Kuhusu bei kwakweli Tecno wameangalia hali halisi ya uchumi kwa sasa ambapo gharama itakuwa kati ya Tsh 500,000 – Tsh 600,000.
Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno nahakikisha hukosi moja wapo ya simuhizi kali ambazo zimekuja kufanya mageuzi ya teknolojia.
0 comments:
Post a Comment