Monday, October 10, 2016

Clinton na Trump watifuana vikali kwenye mdahalo wa pili wa Urais Marekani


Mdahalo wa pili wa Urais nchini Marekani, umefanyika Jumapili hii huko St Louis, Missouri


Wagombea, Donald Trump na Hillary Clinton walitabasamiana lakini hawakushikana mikono walipotambulishwa jukwaani. Mdahalo huo ulianza kwa mjadala iwapo Trump anafaa kuwa amri jeshi mkuu kulingana na jinsi anavyowazungumzia wanawake.
Alirudia kile alichokisema baada ya video ya mwaka 2005 inayomuonesha akiongea maneno ya kudhalilisha wanawake iliyosambaa kwa kudai kuwa yalikuwa mazungumzo ya watu wawili na kwamba hajivunii nayo.

Trump alimgeuzia kibao Clinton kwa kusema kuwa hakuna mtu kwenye historia ya Marekani ambaye amekuwa akidhalilisha wanawake kama mume wake, rais wa zamani, Bill Clinton.
Alisisitiza pia kuwa hakuna namna atajiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho licha ya kuwepo shinikizo ndani ya chama chake cha Republican, wanaotaka nafasi yake ichukuliwe na mgombea mwingine. Mgombea wake mwenza, Mike Pence amesema kuwa hawezi kumtetea Trump.
Baadaye kwenye mdahalo huo, Trump alitishia kumshtaki Clinton dhidi ya matumizi yake ya email alipokuwa waziri wa mambo ya nje kama atachaguliwa kuwa rais, na kuonya kuwa atampeleka jela.
Kwa mujibu wa kura za CNN/ORC, Hillary Clinton ameshinda mdahalo huo wa pili kwa 57% dhidi ya 34% za Trump.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.