Monday, October 10, 2016

Diamond: Ne-Yo, Wizkid, Tekno, Flavour wameipa saluti ‘Salome’

Hit maker wa wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz amemtaja Ne-Yo, WizKid, Tekno pamoja na Flavour kuwa ni miongoni mwa mastaa walioukubali wimbo wake mpya ‘Salome’

Muimbaji huyo amedai kila mmoja kwa wakati wake alivyoona video ya wimbo huo, alionesha kupendezwa na kile alichokifanya.
“Kabla ya wimbo kutoka Wizkid alikuwa Tanzania wakati nipo naye nilimpa ule wimbo aisee ulimvuruga sana, “Diamond alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.
“Hata baada ya wimbo kutoka wasanii wakubwa kama akina Tekno, Flavour walinitumia ujumbe mfupi kuonyesha kupenda, nakumbuka hata Ne-Yo naye aliniambia ‘I like the song.’

Pia muimbaji huyo alisema amepokea salamu za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali akiwemo Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Video ya wimbo huo hadi sasa ina views milioni 4.3 kwenye mtandao wa Youtube.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.