“Nachoomba msiitumie audio mlioconvert kwenye video, audio wengi waliyo nayo ni ile walioconvert kwenye video ambayo sio sawa ina hadi zile sound za sms,” Moe amemuambia mtangazaji wa Ice Fm, Gami Dee.
Alipoulizwa kwanini ameamua kufanya hivyo kwa kuachia video tu, rapper huyo amesema, “Hii ni video yangu ya pili ndani ya miaka kibao iliyopita almost 11, kwahiyo ni kitu ambacho nilitamani siku moja nifanye kuona itasaidia kitu gani. Na kweli kama unavyozungumza naona imepokelewa vizuri.”
Jay Moe amesisitiza redio kusubiri mpaka official audio itakapotoka lakini wasitumie audio iliyo’convertiwa’ na bloggers.
0 comments:
Post a Comment