Wednesday, March 22, 2017

Nicki Minaj Atengeneza Rekodi ya Dunia

Nicki Minaj ametengeneza historia nyingine katika maisha yake ya muziki. Mrembo huyo amefanikiwa kumpiku mkongwe Aretha Franklin kuwa na nyimbo nyingi kwenye Billboard Hot 100 kwa wasanii wa kike duniani.

Franklin ameweka rekodi ya kukalia kiti hicho kwa takribani miaka 40 ambapo kwa alikuwa na nyimnbo 73 katika chati hizo lakini kwa sasa Nicki anashikilia nafasi hiyo akiwa na nyimbo 76 kwenye chati hizo.

Minaj amekalia kiti hicho baada ya hivi karibuni kuachia nyimbo tatu kwa pamoja, ikiwemo ‘No Frauds’ aliyomshirikisha Drake na Lil Wayne, ‘Regret in Your Tears’ na ‘Changed It’ aliyomshirikisha Lil Wayne. Wasanii wengine wanaoongoza katika orodha hiyo ni pamoja na:
76 – Nicki Minaj
73 – Aretha Franklin
70 – Taylor Swift
58 – Rihanna
57 – Madonna
56 – Dionne Warwick
54 – BeyoncĂ©
53 – Connie Francis
48 – Mariah Carey
48 – Brenda Lee
43 – Miley Cyrus
41 – Barbra Streisand
40 – Mary J. Blige
40 – Janet Jackson
40 – Diana Ross
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.