Samatta alianza kuweka kambani dakika ya pili tu tangu kuanza kwa kipindi cha kwanza baada ya kutoka na mpira nje ya box na kuwakusanya mabeki wa Botswana na kuingia nao kwenye box kisha kumtungua kwa mguu wa kushoto golikipa wa Botswana ambaye aliruka bila mafanikio.
Bao hilo lilidumu kwa dakika zote zilizobaki za kipindi cha kwanza huku mchezo ukiwa umechangamka kwa timu zote kushambuliana kwa zamu.
Kipindi cha pili Botswana waliamua kuliandama goli la Stars kwa mashambulizi ya mara kwa mara kwenye goli la Stars na mara kadhaa walipoteza nafasi za kufunga.
Dakika ya 87 kipindi cha pili, Samatta alifunga goli la pili na la ushindi kwa Stars kwa mkwaju wa free-kick nje kidogo ya box la penati baada ya yeye mwenyewe (Samatta) kuangushwa nje kidogo ya eneo la penati box.
Licha ya kufunga magoli mawili, Samatta aliwa kwenye wakati mgumu kwa sababu mara nyingi alikuwa akichezewa rafu zilizosababisha wachezaji wa Botswana kuoneshwa kadi za njano. Samatta ilibidi atibiwe na daktari wa Stars baada ya kufanyiwa rafu wakati akijaribu kumtoka moja ya mabeki wa Botswana.
Umahiri wa golikipa wa Botswana Kabelo Dambe umeisaidia timu yake kupunguza idadi ya magoli kutokana na kuokoa michomo ya miwili ya Mbwana Samatta pamoja na Simon Msuva.
Taifa Stars itacheza tena mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi siku ya Jumanne March 28, 2017 kwenye uwanja wa taifa