Aliyekuwa Waziri wa
Habari, Sanaa, Utamadunu na michezo, Nape Nnauye leo amekabidhi ofisi kwa
Waziri Mpya wa Wizara hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe. Makabidhiano hayo
yamefanyika katika ofisi za Wizara Dodoma.
Aliyekuwa Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye leo amekabidhi rasmi ofisi
kwa Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katika makabidhiano
hayo yaliyohudhuriwa na watendaji wakuu wa Wizara, Mhe. Mwakyembe ameahidi kuwa
licha ya kukabidhiwa ofisi, anaamini kuwa Mhe. Nnauye bado ni mdau mkubwa wa
sekta za Wizara na kuwa anategemea kuendelea kupata ushirikiano kutoka kwake.
Aidha Waziri Mwakyembe
ameahidi kuendeleza yote mazuri yaliyo anzishwa na Nnauye katika kuimarisha
ufanisi wa Wizara na kuhakikisha inakuwa ni moja ya Wizara za mifano nchini.
Amesisitiza kuwa katika kipindi kifupi alichokaa Wizarani, Mhe. Nnauye
alianzisha mabadiliko makubwa na watu wameanza kuifahamu vizuri Wizara.
Kwa upande wake Nnauye
amemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumpa dhamana kubwa ya
kusimamia Wizara kwa kipindi cha miezi 15 huku akiwa ndio kwanza amekuwa mbunge
katika awamu yake ya kwanza. Aidha Nnauye ameahidi kuendela kushirikiana na
Wizara kwa ukaribu kwani ni kweli yeye ni mdau mkubwa wa sekta za wizara hii.