Utafiti mpya uliyofanywa na Chuo Kikuu cha New York, Marekani umegundua mnyama mwingine ambaye ana
ubongo mkubwa sawa na binadamu ambapo utafiti huo ulionesha jinsi gani
mazingira wanayoishi binadamu na Nyani yanavyoshabihiana na kuwafanya kuwa
wanyama pekee wenye ubongo ulio sawa kwa ukubwa.
Mkuu wa utafiti huo Alex Decasian alizungumza
na BBC “Nyani hasa jamii ya Orangutans wana ubongo ulio sawa na binadamu
kwa kuwa hupitia changamoto zinazofanana, nyani mwenye umri mkubwa ana
ubongo mkubwa zaidi kuliko Nyani mtoto, hii inasadia katika ulinzi wa
jamii yao na kutatua matatizo kama ugomvi”
Utafiti huo pia ulionesha nyani
anayekula matunda ana ubongo mkubwa zaidi ukilinganisha na nyani anayekula
majani na mizizi ambapo Mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Oxfordamesema
ubongo mkubwa humtofautisha nyani na wanyama wengine katika uelewa wa mambo,
kuwa na huruma na kutambua majukumu yao.