Monday, April 10, 2017

‘Bunge liahirishwe leo tujadili kuhusu wanaoteka watu’ – Hussein Bashe

Kutoka Bungeni DODOMA, leo April 10, 2017 Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesimama kuomba muongozo kwa Spika wa Bunge akitaka Bunge lisimamishe shughuli za kawaida na kuanza kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea nchini.
Bashe amesema yeye pia ameshatumiwa ujumbe wa vitisho wakimwambia kuna watu 11 akiwemo yeye watafanyiwa vitendo vibaya popote watakapokuwa, hivyo analiomba Bunge lijadili suala hilo kwa dharula kwasababu sio sawa kukaa kimya.
’Kuna watu wamenitumia jumbe za kuniambia kwamba mimi ni kati ya watu 11 ambao tupo hatarini kufanyiwa vitu vibaya na popote pale nijiangalie ninapokuwa barabarani'
Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana' –Hussein Bashe
Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.