Ukiachana na mpenzi wako halafu ukakutana na haya yafuatayo ujue bado unampenda na itakutesa sana hadi uje kumsahau...
#. Mara tu baada ya jamaa/dem wako kukwambia "its over, pls tusisumbuane tena", ukakaa kama dk 10 hivi hlf ukampigia tena simu ukimuuliza, "hivi unamaanisha au? niambie kabisa ohoooo, ujue mimi nikishaamua langu huwa nimeamua!", jamaa/demu akakujibu, "nimeamua", ukakaa dk tano hlf ukampigia tena ukimwambia, "kuwa serious ujue, haya shauri lako!"#. Dalili za kupata maumivu makali ya moyo, ukaanza kuhisi kama unataka kuwehuka hivi, moja haikai, mbili haikai, tatu ndio kabisaaa...unatoka chumbani unaenda sebuleni unashika kile kinyago cha pambo kilichopo juu ya kabati la tv unakiangalia weeee halafu unataka kukibonyeza kuwashia tv ukidhani ni remote
#. Ukisikia simu inaita/ msg imeingia unaianglia simu kwa haraka ikidhani ni yule b/friend au g/friend wako mlioachana amebadilisha mawazo, halafu ukakuta ni simu/msg ya rfk yako uliyesoma nae, ukajikuta unasonya kwa ghadhabu!!!!
#. Kuifungia simu kwenye kabati la nguo ukitazamia kwamba ukija baadae utakuta missed calls/ msgs za huyo uliyeachana nae akiomba radhi, hlf kwa bahati mbaya hukuti missed call wala msg hata moja!!!
#. Kumtumia msg ya kawaida tu ya salamu huyo uliyeachana nae ukijifanya msg uliyomtumia imepotea njia, kwamba ulidhamiria uitume kwa mtu mwingine kbs!
#. Kujifanya una mpenzi mwingine kwa kumtumia msg ya mapenzi huyo uliyeachana nae, ukijifanya ulikua unamtumia mpenzi wako mwingine ili aone wivu, mbaya zaidi uliyemtumia anapiga kimya!
#. Kuchukua simu ya mtu mwingine halafu unampigia huyo ulieachana nae, akipokea unanyamaza huongei halafu unakata!
#. Kumwambia rfk yako ampigie huyo uliyeachana nae ampe taarifa za hatari,,,kama vile unaumwa sanaaa, ili uone response yake!
#. Mengine ongezeeni nyie bwana hahaha