Baada
ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dr. Josephat Gwajima leo April 9,
2017 kumtaka Halima Mdee Mbunge wa CHADEMA kumuomba radhi Spika wa Bunge Job
Ndugai kwa maelezo kuwa alimtukana, jioni hii kupitia Twitter ya Mbunge huyo
ameandika kuhusu kinachoendelea kati yake na Spika Ndugai.
Mdee ameandika
'Namuheshimu sana Mch. Gwajima,sitajibizana nae kwenye mitandao. Niweke
rekodi sawa sijamtukana na wala sitarajii kumkosea heshima Spika.'
Hayo
ya J2 namwachia yeye! Yangu na yaliyojiri Bungeni.. Najua jinsi ya kuyahandle.
Yawezekana yalishamalizwa kabla ya Ibada yake LEO.
Namuheshimu sana Mch.Gwajima,sitajibizana nae kwenye mitandao. Niweke rekodi sawa sijamtukana na wala sitarajii kumkosea heshima Spika. https://t.co/yRxCGcvyPE
— Halima James Mdee (@halimamdee) April 9, 2017
Hayo ya J2 namwachia yeye! Yangu na yaliyojiri Bungeni.. Najua jinsi ya kuyahandle. Yawezekana yalishamalizwa kabla ya Ibada yake LEO. https://t.co/yRxCGcvyPE
— Halima James Mdee (@halimamdee) April 9, 2017