Tuesday, April 25, 2017

‘Mazoea’ Imeniingizia Hela Kuliko Nyimbo Zangu Zote – Billnass

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka label ya LFLG, Billnass amedai wimbo wake ‘Mazoea’ ambao bado unafanya vizuri ndio wimbo uliomwingizia hela nyingi kuliko nyimbo zake zote.

Wimbo huyo aliomshirikisha rapa Mwana FA, umeangaliwa mara 877,121 kupitia mtandao wa YouTube kwa kipindi cha miezi 4.
Akiongea na Bongo5, Billnass amedai ameingiza hela nyingi kupitia shows, ringtone pamoja YouTube.
“Mungu ni mwema sana, ‘Mazoea’ imefanya mambo makubwa sana katika maisha yangu, na ni wimbo ambao umeniingizia hela nyingi sana kuliko nyimbo zangu zote,” alisema Billnass.
Aliongeza, “Mauzo ya mitandaoni yamekuwa makubwa sana, shows nyingi ambazo nimekuwa nikifanya nalipwa vizuri, YouTube. Yaani huu wimbo umekuwa kama baraka katika miasha yangu. Siwezi kusema nimeingiza kiasi gani lakini ni hela nyingi sana,”
Rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio mpya ambao amedai utakuwa na surprises nyingi.

Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.