Tuesday, April 25, 2017

Kamanda Sirro Afafanua Upelelezi Katika Uvamizi Wa Mkutano Wa CUF


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amezungumzia vurugu zilizotokea hivi karibuni katika mkutano uliotakiwa kufanyike na maeneo ya Mabibo na Chama cha wananchi CUF. Kamanda huyo amesema kuwa suala hilo na wale waliojeruhiwa upelelezi utasema kama hao watu ndiyo waliokuja kuvamia au la.

Kamanda Sirro amezungumza na wanahabari na kusema kuwa, mikutano ya ndani inaruhusiwa hata bila kutoa taarifa Polisi, lakini kwa waliojeruhiwa amedai kuwa upelelezi utaweka wazi mengi zaidi.
“Kuna hili tukio lililotokea tarehe 22 mwezi wa 4, 2017 majira ya saa tano karibu na nusu kwenye hotel moja inaitwa Vina Hotel, hii hotel iko maeneo ya Mabibo kuna wanachama wa Chama cha CUF maana yake Chama kile kina kundi A na kundi B inaonekana kundi A walikuwa wanafanya mkutano wao ndani ya ukumbi kwahiyo baadhi ya watu ambao tunafuatilia wakiwa na magari yapatayo mawili walivamia mkutano huo na wakafanya fujo, kwahiyo kukawa na vurugu kubwa sana na baadhi ya watu wameumia lakini huyu bwana Juma Shaban Nkumbi huyu Mwenyekiti wa CUF wanasema wa Kinondoni alikuwa ameita mkutano kwahiyo kwenye vurugu hizo kuna baadhi ya watu wameumia suala kubwa ni kujua kwa wale waliokuja kuvamia walikuja kufanya nini ni suala la upelelezi kwasababu mtu kaumia kakatwa na kitu chenye ncha kali,” alisema Kamanda Sirro.
“Amefungua jalada lake akieleza kuwa amepigwa mtu fulani na huyo mtu ndo kamjeruhi kwahiyo je, ni wale waliovamia ni jambo la upelelezi kwahiyo upelelezi utatuambia kama ni wao waliovamia, nilikuwa nawaambia pale hata kama wamevamia je kuna uhalali wa kumkata na mapanga? ni suala la upelelezi kwahiyo kimsingi niseme tu kwamba wale waliokamatwa nikutokana na yale malalamiko dhidi yao ambapo watu wameandika maelezo yao wamewatambua wamewataja kwahiyo ndiyo kesi imefunguliwa na hili la wao kutujulisha ni suala ambalo kwa kawaida wanamjulisha OCD,” alifafanua Kamanda Sirro.
“OCD wetu ndiyo anaweza kujua hilo lakini nafikiri katika busara ya kawaida mikutano ya ndani mara nyingi huwa siyo lazima tutoe kibali kwa hiyo unaweza kuta vyama vingine vya siasa au madhehebu mbalimbali wanaweza hata wasitupe taarifa kwasababu ni mikutano ya ndani lakini nafikiri kama walifanya busara zaidi watakuwa walimjulisha OCD kama mkutano wa namna hiyo ulikuwa unaendelea.”
Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.