Will Smith amefanya uamuzi huo wa kumkata mtoto wake rasta Jaden Smith ambaye pia ni staa wa
filamu Hollywood.Jaden anajipanga kuigiza filamu ya ‘Life In A Year’ na ili kwenda sawa na uhusika wake alibidi akate nywele. Baada ya Will kuona kuwa dogo analeta ubishi aliamua kuzifyeka mwenyewe
Muonekano mpya wa Jaden
Filamu ya Life In A Year ina kisa cha uhusiano wa kimapenzi kati ya Jaden na Cara Delevingne. Jaden anagundua mpenzi wake ana mwaka mmoja tu wa kuishi na anafanya analoweza kuhakikisha wanaishi kwa furaha na kufanya yote walioota kufanya. Filamu hiyo itaanza kutayarishwa Toronto, Canada