Kamati
ya saa 72 iliyokaa kikao leo April 13 na kuamua kuhusu malalamiko ya Simba kwaKagera Sugar kuhusu
kumtumia mchezaji Mohamed Fakhi katika mchezo dhidi yao April 2 2017
akiwa na kadi tatu za njano kinyume na taratibu na kanuni za Ligi.
Simba walipeleka
malalamiko hayo katika bodi ya Ligi na kuomba ipitie ripoti za waamuzi ili
kujulikana ukweli, leo April 13 kamati ya saa 72 chini ya mwenyekiti wake Hamadi
Yahayailikaa na kujiridhisha kuwa Kagera walikiuka taratibu hizo kwa mujibu wa
Kanuni Simbawamepewa
point zote tatu za mchezo dhidi yao.
Kamati
imejiridhisha kuwa mchezaji Mohamed Fakhi alioneshwa kadi za njano katika mchezo
dhidi ya Majimaji, Mbeya
City na African
Lyon, hivyo hakustahili kucheza katika mchezo dhidi ya Simba uliyochezwa April 2 2017 uwanja wa Kaitaba na Simba ikapoteza kwa magoli 2-1.