Polisi takriban saba wameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kupigwa risasi huko Mkuranga mkoani Pwani.
Taarifa za awali zimedai kuwa polisi hao walikuwa wakijianda kutoka doria ya barabarani na kurudi kituoni. Vyanzo vimedai kuwa majambazi hayo yalilishambulia gari walimokuwa kwa kumpiga risasi dereva na gari kupinduka kabla ya kuwamiminia risasi polisi sita na kuwaua pale pale.
Bunduki walizokuwa nazo aina ya SMG zimeporwa. Taarifa zingine zimedai kuwa mauaji hayo yamefanywa na mtu mmoja aliyekuwa na silaha nzito.