Akiongea na kipindi cha Dj Show cha Radio One, kitendo hicho kimeonyesha kumfurahisha kinda huyo
Kutoka lebo ya WCB ambao ni mahasimu wakuwa wa hitmaker wa Aje.
“Nimefurahi sana kwa sababu wale ndio watu walioanza muziki kitambo na ukiona wanapenda unachokifanya inaonyesha njia nzuri uendelee kukaza ili uendelee kuwagusa mashabiki wengi. Inanipa moyo niendelee kukaza zaidi na zaidi,” amesema Rayvanny.
Hii ni hatua nzuri kwa Ray kwani alishawahi kusema hakuna tatizo hata akifanya wimbo na Alikiba japo hawapikiki chungu kimoja na bosi wake.