Sunday, September 24, 2017

Serikali kuwabana wakala wa vyuo vikuu vya nje ya nchi


Tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU), imesema tayari kuna sheria na wanadhibti wakala ama wawakilishi wa vyuo vikuu vya nje ya nchi wanakokwenda kusoma elimu ya juu vijana wa Kitanzania, ambapo kubwa ni sifa za kusoma vyuo hivyo iwe sawa na ya kusoma vyuo vya nchini.

Afisa habari mwandamizi wa TCU, EDWARD MKAKU, ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi zaidi ya 200 wanaotarajiwa kuondoka nchini Septemba 27 mwaka huu, kwenda Marekani, Ulaya, Asia na Afrika Kusini, katika vyuo vinavyowakilishwa hapa nchini na Universal Abroad Representatives (UAR), ambapo amewatoa hofu wazazi wa watoto husika, kuwa TCU, inawatambua wawakilishi hao.


Kwa upande wake TONY KABETHA, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa Taasisi hiyo inayoviwakilisha vyuo vya nchi za Marekani, Australia, China, Norway, Canada, Uingereza, Sweden, Denmark na India, amesema, wanafunzi hao wote shahada zao za kwanza zitajikita katika masuala ya teknolojia za viwanda pamoja na sekta ya mafuta na gesi, zinazotarajiwa kuwa chachu ya uchumi wa Tanzania.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.