Friday, April 14, 2017

Ndoa ya Lulu na Majay Yanukia

Elizabeth Michael (Lulu) amedai ndoa yake na mpenzi wake Dj Majay inakaribia.

Muigizaji huyo ambaye ameonekana kutulia sana tangu alipokuwa na mahusiano na bosi huyo wa EFM
na TVE amesema hivi karibuni wale waliokuwa wakitaka waachane watabaki midomo wazi.
“Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo wa Mungu. Hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni,” ameliambia gazeti la Mtanzania.
Lulu ameongeza kuwa anatamani kuwa mke bora kwenye ndoa yake kama alivyokuwa sasa kwenye mahusiano yake.

Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.