Jioni
ya April 12 2017 staa wa muziki wa hip hop bongo Hamisi
Mwinjuma ambaye wengi tunamfahamu kwa jina la Mwana
FA, alitoa taarifa kupitia ukurasa wake wa twitter kuoneshwa
kufurahisha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John
Pombe Magufuli kumpigia
simu.
Mwana
FA ambaye kwa sasa
anafanya vizuri katika radio na tv stations mbambali kwa hit single yake ya Dume Suruali amethibitisha
kupigiwa simu na Rais kumwambi anakubali kazi zake.
Kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa
staa huyo uliyokuwa verified aliandika “nimefurahi kupokea simu ya
Mheshimiwa Rais @MagufuliJP kunisalimia na kuniambia yeye
ni mpenzi wa kazi zangu,haswa #DumeSuruali..”