Friday, April 14, 2017

Nuh Mziwanda–Last Born Records Ni Urithi Nitakaouacha Hata Kwa Vizazi Vijavyo

Nuh Mziwanda amesema label yake, Last Born records si kwaajili yake pekee. Amesema hata siku akiwa ametoweka duniani, itaendelea kuwepo na ndio maana anaendelea kukusanya jeshi.


“Nataka nikizeeka au nikiwa sipo duniani basi niwe nimeacha watu wa kunikumbuka au vitu ambavyo vitakuwa kwenye historia ya maisha yangu, that’s why hivi sasa kwenye studio yangu Last Born records Nina wasanii wawili wapya kabisa ambao ntawatambulisha baada ya miezi miwili au mitatu ijayo,” amesema muimbaji huyo.
“Mmoja anaitwa Chichi Chadala, huyu yeye anaimba muziki wa kurap na mwingine anaitwa Computer, huyu yeye anaimba na huyu computer ndiye kaandika wimbo wangu wa Anameremeta, “ Mziwanda alikiambia kipindi cha VMix cha Channel 10.
Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.