Tuesday, September 6, 2016

Fella Akwama: Juma Nature Hanitaki Anaona Sina Maana’

Mkurugenzi wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family, Mkubwa Fella ameonekana kugonga mwamba juhudi zake za kutaka kurudisha mahusiano yake ya kazi na msanii wake wa zamani wa Kundi la TMK Family, Juma Nature.


Hapo awali Juma Nature alikuwa msanii wa Kundi la TMK Wanaume Family la Mkubwa Fella lakini baadae aliondoka na kwenda kuanzisha Kundi lake la TMK Wanaume Halisi. Akiongea  Ijumaa hii, Fella amedai wasanii ambao wanamthamini ni wale ambao yupo nao.
“Mimi ndo hanitaki, anaona mimi sina maana, lakini walioona mimi na maana ndo hawa ambao nipo nao mpaka sasa,” alijibu Fella baada ya kuulizwa kama ana mpango wowote na Juma Nature kwa sasa.Kauli hiyo inaonyesha meneja huyo ameonga mwamba juhudi zake za kutaka kumrudisha msanii huyo kundini baada ya
kuhaidi mara kadhaa kufanya hivyo
Share:

Joh Makini na msanii wa Nigeria, Falz kuungana kwenye Coke Studio Africa msimu wa 4

Msanii wa Hip Hop Bongo, Joh Makini yupo nchini Nairobi, Kenya akiwa ni miongoni mwa wasanii wanne watakaoiwakilisha Tanzania kwenye kipindi cha Coke Studio Africa Season 4.


Huu ni msimu wa pili kwa rapper huyo wa Bongo kushiriki kwenye kipindi hicho. Kwa msimu wa tatu, Joh Makini aliungana na msanii wa Nigeria, Chidinma ambaye walitengeneza mchanganyiko uliowavutia mashabiki wa kipindi hicho kitu kilichopelekea mpaka wakafanya collabo ya wimbo wa ‘Perfect Combo’.


Kwa msimu huu Joh Makini ameungana na rapper wa Nigeria, Falz ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Chardonnay Music’ lakini ikiwa ni msimu wake wa kwanza kushiriki kwenye kipindi hicho.

Huu ni wimbo wa Falz, ‘Chardonnay Music’ ambao ameuachia wiki iliyopita.
Share:

Ben Pol Asisitiza Kuitoa Album Yake Mwaka Huu

Ben Pol amedai kuwa mpango wa kutoa album yake mwaka huu upo pale pale.

Ameiambia Bongo5 kuwa album hiyo imechelewa kutoka kwasababu yeye na uongozi wake wanatengeneza mkakati wa kuipromote na kuiuza ili iende mbali na kumfikia kila shabiki aliyenuiwa.

Hata hivyo muimbaji huyo wa ‘Moyo Mashine’ amedai kuwa lengo la kuitoa si kupata fedha bali ana sababu zingine kuu mbili.
“Moja ni kutengeneza ukamilifu wa mwanamuziki,” anasema Ben.
“Mimi si mtu wa magumashi, kama unataka ukamilifu wa kuitwa mwanamuziki au msanii uliyekamilika, lazima uwe na album,” ameongeza.

“Lakini pili, nataka baadaye biashara ya album ikirudi kuwa stable, ikija kuwa ni deal yaani, niweze kuwa katika watu ambao walithubutu kutoa album licha biashara kuwa bado si nzuri, Ben Pol alikuwepo, kwahiyo niingie kwenye wale wanaharakati waliothubutu kurudisha biashara ya album regardless ya situation ya mauzo ya kipindi hicho au situation ya biashara yenyewe kwa ujumla.”

“Kwahiyo watu wategemee album yangu mwishoni mwa mwaka huu mzigo utatoka.!
Share:

Mkhitaryan Hana Uhakika Kama Atacheza Derby

Kiungo wa Manchester United na timu ya Taifa ya Armenia Henrikh Mkhitaryan hana uhakika kama atacheza Manchester Derby baada kuumia katika mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Czech jumatano iliyopita.

Henrikh Mkhitaryan kupitia akaunt yake ya twitter alipost ujumbe huu

Not sure yet if I’ll bit fit for the derby, but I’m motivated as ever to put all energy to be in great shape asap!!
Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.