Tuesday, September 6, 2016

Kuizawadia Taifa Stars Dola 10,000 Za Marekani TFF Watuma Salamu Za Shukrani Kwa Gavana Wa Nigeria Kwa

Taifa Stars ilicheza mechi hiyo Jumamosi Septemba 3, 2016 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017). Katika mchezo huo ambao mashabiki waliingia bure, Taifa Stars ilifungwa bao 1-0 mara baada ya kuibana Super Eagles hivyo kumsukuma Gavana huyo kuandaa hafla ya chakula cha jioni ambako mbali ya kuizawadia Stars, pia aliizawadia Super Eagles dola 35,000 za Marekani.

Taifa Stars ilitua Dar es Salaam usiku wa kuamkiia leo Septemba 5, 2016 ambako baadhi ya wachezaji walipelekwa Hoteli ya Urban Rose, iliyoko katikati ya Jiji la Dar es Salaam wakati wengine hususani wale wa timu ya Azam FC walichukuliwa na viongozi wao kwa ajili ya safari ya kwenda Mbeya ambako Jumatano wanatarajiwa kucheza na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaofanyika Uwanja wa Sokoine mjini humo.
Kadhalika wachezaji wa Young Africans nao walichukuliwa kwa ajili ya safari ya kwenda Mtwara ambako watakuwa na mchezoi dhidi ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini humo wakati nyota wa Simba watabaki hapa Dar es Salaam kwani Jumatano itakuwa na kibarua dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Wakati nyota 18 wakitua Dar es Salaam, Nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta aliishia Nairobi, Kenya ambako aliunganisha ndege ya kwenda Brussels, Ubelgiji.
Licha ya mchezo huo kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini ulikuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kwa fainali hizo kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.
Wachezaji waliotua ni
Makipa-
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC
Mabeki
Vicent Andrew – Young Africans
Mwinyi Haji – Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe – Azam FC
David Mwantika – Azam FC
Viungo
Himid Mao – Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi – Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania
Washambuliaji
Jamal Mnyate – Simba
Simon Msuva – Young Africans
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco – Azam FC
Mbwana Samatta –KRC Genk ya Ubelgiji
Viongozi waliofika Dar ni:
Ahmed Mgoyi – Mkuu wa msafara
Charles Boniface Mkwasa- Kocha Mkuu
Hemedi Morocco – Kocha Msaidizi
Hussein Swedi – Mtunza Vifaa
Richard Yomba – Daktari wa timu
Share:

Kinachowarudisha Nyuma Baadhi Ya Rappers Wa Bongo Ni Hiki

Tanzania imebahatika kuwa na rappers wakali kwa uandishi na wenye uwezo mkubwa wa kutumia kalamu zao kucheza na lugha watakavyo.

Lakini ni rappers wachache tu wanaofaidi matunda ya jasho lao. Ni wachache tu wanaopokea simu kutoka kwa mapromota wanaowaita kwaajili ya show. Ni waimbaji pekee ndiyo wanaoendelea kufaidi na tena inashangaza hata waimbaji wachanga tayari wameingia kwenye orodha ya wasanii walio busy kwa show, pesa kibao zikiwafukuzia.

Lakini kuna kitu ambacho waimbaji wanacho, kinachowasaidia kuwafanya wawe karibu na mashabiki wa kila rika ukilinganisha na wachanaji. Waimbaji wengi wamekuwa na nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi ambao hugusa hisia za mashabiki moja kwa moja.
Haimaanishi kuwa rappers nao wanapaswa kuanza kuimba mapenzi pekee kwenye nyimbo zao, bali kuimba vitu vinavyohusisha maisha ya mashabiki. Mapenzi, Matatizo, Stress, Umaskini, Kusalitiwa, Ukosefu wa Ajira, Majaribu, Imani, Maisha ya kila siku, Pesa, Urafiki, Ugomvi, Kula bata, Warembo, ni miongoni mwa mambo yanayowahusu wananchi ambayo kama wimbo ukiyagusa hayo, ni lazima wimbo ufanye vizuri.
Share:

Rooney Aweka Rekodi Mpya Timu Ya Taifa Ya England

Huu ulikuwa ni mchezo wake wa 116 kuiwakilisha England ilipokutana na Slovakia katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2018.
David Beckham ndiye alikuwa anashika rekodi hii kwa kucheza mechi 115 lakini kwasasa Rooney ameipita hiyo ya Beckham na kuandika yake ya kucheza mechi 116.

Mlinda mlango Peter Shilton, ndiye anaishika rekodi ya jumla kwa kuichezea England mara 125.
Share:

Monday, September 5, 2016

Uganda Yafuzu Afcon 2017 Kwa Mara Ya Kwanza Tangu 1978

Timu ya taifa Uganda imefuzu katika fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika 2017 baada ya miaka 38, The Cranes walishinda 1-0 dhidi ya Comoro siku ya Jumapili, ushindi ambao umewafanya kutimiza pointi 13 zilitosha kuwapa tiketi ya AFCON 2017.


Goli la Uganda limefungwa na Farouk Miya mbele ya mashabiki kibao wa Uganda jijini Kampala.

Mara ya mwisho The Cranes kucheza Afcon ilikuwa mwaka 1978 ilipofanikiwa kufika hadi fainali na kufungwa na Black Stars ya Ghana.
Mataifa 16 yatashiriki michuano hiyo itakayoandaliwa 14 Januari hadi 5 Februari. huko Nchini Gabon.
Timu zilizofuzu mpaka sasa. #AFCON2017




Share:

D’Banj: Ndoa Yangu Haiwahusu, Niacheni!

Wiki kadhaa zilizopita, D’Banj alitengeneza vichwa vya habari baada ya kudaiwa kuwa amefunga ndoa kisiri na mpenzi wake, Lineo Didi Kilgrow.





















Tangu hapo, muimbaji huyo amekuwa kimya kuhusiana na suala hilo hadi Jumamosi iliyopita alipozungumza na Saturday Beats.
Akizungumza kuhusu ndoa yake, muimbaji huyo alisema maisha yake binafsi hayahusianI na mtu yeyote na kuwaomba watu kuyaacha maisha ya familia yake faragha.
“Ndoa yangu ni mambo yangu na si mambo ya mtu mwingine. Kama nimeoa ama sijaoa, fuatilia mambo yako. Kama ukija kuona pete ya ndoa kwenye kidole changU, sawa, lakini kama huoni, sawa,” alisema.
“Ukweli kuhusu hilo ni kwamba ni muhimu sana kujua unachotaka kama brand. Kama brand, nilitaka kujikita kwenye upande wa biashara na kuweka familia na maisha binafsi faragha,” aliongeza msanii huyo.
Staa huyo anatarajia kuachia album yake mpya iitwayo CREAM.
Share:

Mr Blue Kumpeleka Mahakamani Anayejaribu Kuharibu Ndoa Yake

Mkali wa wimbo ‘Mboga Saba’ Mr Blue ambaye  hivi karibuni alipatwa na msukosuko wa kuyumba kwa ndoa yake, kutokana na kusambaa kwa tetesi za kuwasiliana na ex wake Najma, amesema yuko tayari kumchukulia hatua za kisheria aliyesababisha ugomvi huo.



Rapper huyo amesema yeye binafsi hakuwasiliana na Naj, isipokuwa habari hizo zilipoanza alidhani ni kiki inayotengenezwa na Naj pamoja nampenzi wake Barakah The Prince, ili kuachia wimbo wao wa pamoja.
“Ile habari ilikuwa ya uongo, mwanzoni mi nilihisi Barakah na mchumba wake Najma watakuwa wameitengeneza kwa ajili ya mambo yao ya kutafuta kiki, kwa sababu ilisemekana kuna nyimbo yao wanataka kutoa Barakah na Najma, kwa hiyo wanatafuta kama kiki kutumia ubavu wangu, nikabahatika kukutana na Barakah na kumshika mkono, na kumwambia akubali mbele za watu, akasema hajui hiyo taarifa”, Mr Blue alikiambia kipindi cha Planet Bongo.

Aliongeza,”Hatua za kisheria lazima zichukuliwe unajua hivi vitu sio vitu vya kuharibiana, mi sa hivi nishakuwa mtu mzima, siwezi kurudia matapishi ambayo nishawahi kuyatapika, eti nikampigie Najma sijui niwe naye, kwa sababu mimi najua mke wa kumuoa najua mwanamke wa kuwa naye ndio maana nikamchagua mke wangu, na nampenda na amenizalia watoto wazuri, kwa hiyo siwezi tena kufikiria eti kumpigia Najma, siwezi kufikiria kugombana na Barakah The Prince, kwanza hatulingani, mi wakati naanza mziki ye bado yuko shule anasoma, kama ni kweli ni wao japokuwa Barakah amenithibitishia sio wao, nikijua ni wao lazima nitafute njia ya kuwashikisha adabu.”
Share:

Copyright © TODAY'S YOUTH FOUNDATION | Designed by Francis Ikomba Distributed By Norbert Inc.